Home Soka Zahera Kufungua Akademi

Zahera Kufungua Akademi

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha wa Yanga sc Mwinyi Zahera ana mpango wa kufungua akademi ya michezo maalumu kwa vijana wa miaka 9 na kuendelea ili kuwakuza na baadae kuwauza katika timu kubwa nchini na nje ya nchi.

Zahera aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano na baadhi ya stesheni za redio hapa nchini wakati akijibu tuhuma mbalimbali kuhusu kufukuzwa ajira yake katika klabu ya Yanga na mustakali wake hapa nchini.

“Kesho naenda Kongo kujiunga na timu ya taifa kujiandaa na Afcon dhidi ya Gabon na baada ya mechi nitarudi hapa Tanzania,Mimi nawapenda sana mnavyoishi hapa nitawekeza hapa nchini nataka kufungua akademi ya mpira wa miguu”.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited