Home Soka Zayd,Edmund Waitwa Stars

Zayd,Edmund Waitwa Stars

by Dennis Msotwa
0 comments

Wachezaji Yahya Zayd wa Azam Fc na mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga sc wamekua ni moja ya majina ya mastaa walioitwa na kocha Hemed Morroco kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuelekea michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Niger na Congo Brazaville inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka huu.

Katika kikosi hicho chenye mastaa 23 ambao wameitwa kuingia kambini kuanzia jumanne ya 2/9/25 ambapo kocha Hemed Morroco amewaita kwenda kutoa mchango wao katika maeneo ya kiungo kwa Zayd sambamba na eneo la ushambuliaji kwa Edmund John ambapo mastaa hao wote hawakuitwa katika kikosi kilichoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).

Zayd,Edmund Waitwa Stars-sportsleo.co.tz

banner

Mastaa wengine ambao hawakuwepo katika kikosi cha Chan lakini wameitwa ni Mbwana Samata,Simon Msuva,Charles M’mombwa,Novatus Dismas,Anthony Remmy na Seleman Mwalimu ambapo wengi hawakuitwa kutokana na kuchezea timu za nje ya Tanzania hivyo kukosa sifa ya kujiunga na Chan ambapo Tanzania tulitolewa hatua ya robo fainali na Morocco.

Kwa mujibu wa ratiba kutoka Shirikisho la soka barani Afrika (Caf),Stars ilipaswa kucheza Septemba 5 2025 dhidi ya Congo Brazaville huku pia ikitarajiwa kurudi tena uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Niger 9 Septemba 2025 na kisha kambi hiyo itavunjwa na mastaa hao kurudi katika vilabu vyao.

Katika msimamo wa michuano hiyo Tanzania ipo katika kundi D ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama tisa katika michezo mitano huku Morocco wakiwa vinara wakikusanya alama 15 katika michezo mitano ambayo wameshinda michezo hiyo yote na Zambia na Niger zenyewe zote zipo nafasi ya tatu na nne zikiwa na alama sita huku Congo Brazaville na Eritrea zenyewe zikiwa hazina alama.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa mchezo baina ya Tanzania na Congo Brazaville usiwepo kutokana na nchi hiyo kufungiwa na shirikisho la soka Duniani (Fifa) kutokana na Serikali ya nchi hiyo kuonekana moja kwa moja kuwa inaingilia masuala ya michezo kinyume na sheria na taratibu za Fifa kwa nchi wanachama.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited