Home Makala Feisal Atemwa Stars

Feisal Atemwa Stars

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Feisal Salum ameachwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya msuli mkubwa wa mguu.

Kiungo huyo kipenzi cha wanayanga alikua na majeraha ya msuli tangu mwezi january ambapo alikaa nje kwa kipindi cha siku kadhaa lakini sasa ameyatonesha majeraha hayo hivyo anarejea klabuni Yanga sc kutafuta utimamu wa mwili pamoja na matibabu zaidi.

Daktari wa timu ya Taifa ya Tanzania Dk.Lisobine Kisongo amesema kuwa mchezaji huyo amejitonesha jeraha lake aliloumia tangu january mwaka huu hivyo kwa maendeleo ya mchezaji na nchi kwa ujumla hawana budi kumruhusu kujiunga na klabu yake kwa matibabu zaidi.

banner

Feisal ni mchezaji muhimu kwa klabu yake ya Yanga sc na timu ya Taifa ya Tanzania kutokana na kiwango chake huku klabu ya Yanga sc ikimtegemea zaidi kuelekea katika michezo muhimu dhidi ya Azam Fc na Simba sc ambayo itaamua hatma ya ubingwa wa ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited