Mkataba wa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza umebakisha siku 39 kutamatika huku klabu hiyo ikiwa bado na mechi kadhaa za ligi kuu kabla ya msimu kuisha.
Ntibanzokiza licha ya mkataba wake kuelekea kuisha ameibuka kama mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga sc ambapo mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 6 na kutoa usaidizi wa mabao kadhaa klabuni hapo akichuana kwa ukaribu na Fiston Mayele mwenye mabao 11 ya ligi kuu nchini.
Saido alijiunga na Yanga sc kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu baada ya kuonekana katika mchezo kati ya Tanzania na Burundi aliwahangaisha viungo wa Stars akiwemo Jonas Mkude ambaye alipewa kadi nyekundu katika mchezo huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mchezaji huyo ni kati ya mastaa ambao mikataba yao inaisha msimu huu klabuni hapo japo wa kwake utaisha huku ikiwa ligi kuu haijaisha na tayari Mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga sc Senzo Mazingisa amesisitiza kuwa suala hilo lipo mikononi mwa kocha Nasredine Nabi akisubiriwa kutoa ruhusu ili mchezaji huyo aongeze mkataba.