Home Makala Simba sc Yamalizana na Phiri

Simba sc Yamalizana na Phiri

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambulia wa klabu ya Zanaco Fc Moses Phiri raia wa Zambia kwa mkataba wa miaka miwili ambapo hivi sasa inasubiri kumtambulisha tu baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.

Klabu hiyo mabingwa wa ligi kuu nchini mara 18 ilifanikiwa kumsainisha mkataba wa awali staa huyo tangu mwezi wa nne mwaka  huu na sasa tayari imemsainisha mkataba wa miaka miwili ikisubiri amalize mkataba wake na klabu ya Zanaco Fc ili imsajili moja kwa moja ambapo atakuja kuchukua nafasi ya Chriss Mugalu ambaye anatemwa akimaliza mkataba wake msimu huu.

Mshambuliaji huyo pia alikua anatakiwa na klabu ya Yanga sc ambapo mmoja wa mabosi wa juu wa klabu hiyo alikwenda mpaka nchini Zambia kufanya mazungumzo na mchezaji huyo lakini hawakufikia muafaka na sasa anatua kwa wapinzani wao Simba sc.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited