Home Makala Namungo Yatolewa Mapinduzi Cup

Namungo Yatolewa Mapinduzi Cup

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Namungo Fc imetolewa katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-4 kutoka kwa Mlandege katika changamoto ya mikwaju ya penati baada ya awali kutoka 1-1 katika dakika tisini za mchezo.

Iliwachukua Namungo Fc dakika saba pekee kuandika bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Mkoko kwa kichwa baada ya mabeki wa Mlandege Fc kuzembea kuokoa krosi iliyopigwa kutoka upande wa kushoto mwa uwanja.

Dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza Mlandege walisawazisha bao hilo kupitia kwa Bashima Saite baada ya kipa wa Namungo kuutema mpira uliopigwa langoni kwake na mfungaji kuuwahi mpira huo na kufunga kirahisi ambapo licha ya mashambulizi ya hapa na pale mpaka dakika tisini zinakamilika matokeo yalibaki hivyo hivyo.

banner

Changamoto ya mikwaju ya penati Mlandege Fc walifanikiwa kufunga zote tano huku Namungo Fc wakikosa penati moja na kuwafanya Mlandege Fc kuungana na Singida Big Stars kucheza mchezo wa fainali wikiendi hii siku ya Ijumaa Januari 13.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited