Home Makala Kmc Chali kwa Geita Gold Sc

Kmc Chali kwa Geita Gold Sc

by Sports Leo
0 comments

Mabao mawili ya Elias Maguri na Godfrey Julius yalitosha kuipa alama tatu Geita Gold Sc dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Maguli mshambuliaji wa zamani wa Simba sc alifunga bao kali dakika ya pili ya mchezo huo akipiga shuti la mbali akiwa pembeni mwa boksi la mita kumi na nane na kumuacha kipa wa Kmc akiwa hana la kufanya huku beki Andrew Vicent akiwa amechelewa kuucheza mpira huo.

Dakika ya 81 Kmc walifungwa tena bao la pili na Godfrey Julius na kuihakikishia alama tatu Geita Gold sc ambao kutokana na ushindi huo sasa wamefikisha alama 37 katika nafasi ya tano na Kmc wakiwa na alama 26 katika nafasi ya 14 hatarini kushuka daraja.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited