Home Makala Simba sc Yaishangaza Afrika

Simba sc Yaishangaza Afrika

by Sports Leo
0 comments

Haikutegemewa kama klabu ya Simba sc itaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya klabu ya Wydad Ac katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika uliofanyika nchini siku ya Jumamosi April 23 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Ikiingia kama “Underdog” Simba sc ilianza na kikosi kilichoimaliza Yanga sc huku kikiwa na mabadiliko ya eneo la kiungo ambapo Sadio Kanoute alichukua nafasi ya Erasto Nyoni huku wageni wakiwakosa takribani nyota wanne wa kikosi cha kwanza.

Jean Baleke alifunga bao pekee la mchezo huo dakika ya 41 kipindi cha kwanza akimalizia shuti kali la Kibu Dennis ambapo pamoja na timu kurudi kipindi cha pili bado mchezo ulikua mgumu upande wa Wydad Ac kuweza kupata bao la kusawazisha.

banner

Mpaka dakika tisini za mchezo huo zinakamilika Simba sc ilifanikiwa kumaliza kwa ushindi na kutanguliza mguu mmoja nusu fainali hatua ambayo kwa miaka ya hivi karibuni hawajawahi kufika na sasa watalazimika kupambana katika mchezo wa pili nchini Morocco wikiendi ijayo ili kufika hatua hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited