Home Makala 270m Yamng’oa Feisal Yanga sc

270m Yamng’oa Feisal Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Imefahamika kwamba klabu ya Azam Fc imelipa kiasi cha shilingi milioni 270 ili kupata huduma ya kiungo Feisal Salum kutoka klabu ya Yanga sc nje ya dau la usajili alilochukua staa huyo.

Azam Fc imempa mkataba wa miaka minne staa huyo huku akivuta mshahara wa shilingi milioni 14 sambamba na dau zito la usajili ambapo jumla dili hilo limewagharimu Azam Fc zaidi ya shilingi milioni mia tano kumnasa staa huyo.

Licha ya Yanga sc kuweka ngumu kumuuza Feisala hasa baada ya kugoma na kuondoka kambini ilibidi juhudi kubwa zitumike kumaliza sakata hilo huku Azam Fc mwanzoni wakiweka ofa ya milioni 160 ambazo Yanga sc walizikataa na hatimaye kukubaliana kiasi tajwa.

banner

Pamoja na kiasi hicho pia kuna kipengele cha kumzuia mchezaji huyo asiende Simba sc iwe kwa kumuuza ama kwa mkopo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited