Home Makala Yanga sc Yaizidi Ujanja Azam Fc

Yanga sc Yaizidi Ujanja Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la ngao ya jamii uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Yanga sc ikianza na kipa Djigui Diara na mabeki Yao Kuoasi,Bakari Mwamnyeto,Ibrahim Hamad na Joyce Lomalisa huku eneo la kiungo ikiwaanzisha Mudathir Yahya,Khalid Aucho,Farid Musa na Skudu Makudubela huku ikianza na mashambuliaji mmoja Kennedy Musonda ilifanikiwa kuwamiliki Azam Fc iliyokua na viungo James Akaminko,Sospeter Bajana na Feisal Salum huku mchezo ukiwa wa kukamiana zaidi.

Kipindi cha pili kilimalizika matokeo yakiwa suluhu na uamuzi wa kocha Miguel Gamondi wa kuwaingiza Stephan Aziz Ki na Clement Mzize ulibadili kasi ya mchezo kwa Yanga sc na kusababisha kupata mabao mawili ya haraka kupitia kwa Aziz Ki 84′ na Mzize 89′.

banner

Yanga sc sasa itakutana na Simba sc katika mchezo wa fainali utakaofanyika siku ya jumapili August 13 katika uwanja huo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited