Home Makala “Derby Haitabiriki” Robertinho

“Derby Haitabiriki” Robertinho

by Sports Leo
0 comments

Kocha mkuu wa klabu ya Simba sc Roberto Oliveira maarufu kama Robertinho amesema kuwa hana hofu na mechi ya fainali ya watani wa jadi ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga sc kwa maana mchezo huo huwa hautabiriki licha ya kikosi cha kufanya maandalizi ya kutosha.

Robertinho amesema hayo wakati wa mkutano na wandishi wa habari uliofanyika jijini Tanga ikiwa ni utaratibu maalumu wa kuongea na vyombo vya habari kabla ya mchezo.

“ Derby ni Derby na siku zote haitabiliki. Tunafahamu itakuwa mechi ngumu na tunaiheshimu Yanga lakini tupo tayari kuhakikisha tunashinda. ”

banner

“ Nimeiandaa timu yangu kucheza vizuri wakati hawana mpira, kucheza kwenye eneo la mpinzani, kushambulia kwa nguvu, kufunga magoli na kufurahia mchezo l badala ya kucheza kwa stress, mwisho wa yote, ushindi ndilo lengo letu, ”Alisema Robertinho

Mchezo unatajwa kuwa na presha kubwa kutokana na ukweli kwamba timu zote zimepania kuanza msimu vizuri kwa kutwaa kombe la kwanza hasa kwa upande wa Simba sc ambao hawajatwaa taji hilo kwa takribani misimu miwili mfululizo huku Yanga sc nao wakitaka kulitwaa kwa mara ya tatu mfululizo.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited