Home Makala Beki Simba sc Apata Ajali

Beki Simba sc Apata Ajali

by Sports Leo
0 comments

Beki wa klabu ya Simba sc Che Fondoh Malone amepata ajali usiku wa kuamkia jumapili akitoka uwanja wa ndege wa J.K Nyerere kuwapokea baadhi ya wanafamilia wake waliokuja kumtembelea wakitokea nchini Cameroon.

Malone katika tukio hilo hakuumia sehemu yeyote ile lakini mmoja wa watu waliokuwapo katika gari hilo aliumia mkono na aliwahishwa hospitali mara moja kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Chanzo cha ajali hiyo kwa mujibu wa mashuhuda ni kuwa derev alikua anajaribu kumkwepa mwendesha pikipiki aliyeingia barabarani bila kuchukua tahadhari.

banner

“Ni kweli mchezaji wetu Che Fondoh Malone usiku wa kuamkia jana alipata ajali maeneo ya karibu na mbezi alipokua akitoka uwanja wa ndege kuwapokea ndugu zake waliokuja kumsalimia huku chanzo cha ajali ni dereva bodaboda kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari na sasa tayari yuko nyumbani na hajaumia”Alisema Ahmed Ally meneja habari wa klabu ya Simba sc.

Malone ndani ya uwanja amekua mchezaji wa kutegemewa tangu asajiliwe klabuni hapo msimu huu akicheza pacha ya mabeki wa kati sambamba na Henock Inonga Baka.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited