Mastaa watatu wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri wapo hatihati kuivaa Yanga sc katika mchezo wa hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika utakaofanyika nchini siku ya Jumamosi Disemba 2 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo Gamal Gabr amesema kuwa mastaa hao ni Taher Mohamed, Antony Modeste na Mahmoud Metwaly wanaweza kuukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Pia Gabr amebainisha kuwa klabu hiyo inaweza kuingia nchini jioni ya leo Novemba 30 tayari kwa mchezo huo ikiwa na kikosi cha wachezaji 25 wakiwemo mastaa Percy Tau na Mohmoud Kahrabah.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc inatakiwa kushinda mchezo huo dhidi ya mabingwa hao wa bara la Afrika ili kujitengeneza mazingira mazuri ya kufuzu robo fainali kutokea katika kundi D ambapo mchezo wa mwisho ilikubali kipigo cha 3-0 kutoka kwa CR Belouzdad.