Timu ya Taifa ya Misri imeanza vizuri michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao moja kwa bila dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya hiyo uliochezwa jana usiku.
Wenyeji wakiongozwa na mshambualiaji hatari anayeichezea Liverpool ya Uingereza Mohamed Salah walianza mchezo kwa mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa zimbabwe japo walikosa nafasi kadhaa za kufunga magoli.
Iliwalazimu wenyeji kusubiri mpaka dakika ya 41 kipindi cha kwanza kupata bao lililiwekwa kimiani na mshambualiaji Mahmoud Trezeguet anayeichezea klabu ya Kasimpasa ya nchini Uturuki.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo kinyume na matarajio ya wengi mshambualiaji Mohamed Salah alishindwa kufumania nyavu katika mchezo huo huku kwa upande wa Zimbabwe Kalma Billiat akifanikiwa kuwasumbua wenyeji.