Home Soka Chama Atambulishwa Yanga sc

Chama Atambulishwa Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Mapema asubuhi ya leo klabu ya Yanga sc imemtambulisha kiungo mshambuliaji Cletous Chama kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo akijiunga kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine akiwa huru baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Simba sc.

Awali taarifa za Chama kujiunga na Yanga sc zilikua nyingi huku ikisemekana kuwa Simba sc walikosa maamuzi ya moja kwa moja ambapo baadhi ya mabosi wakitaka aongezwe na wengine wakitaka aachwe kutokana na kukosa nidhamu kikosini humo.

Yanga sc ilitumia nguvu kubwa ya ushawishi wa kifedha kumsajiri Chama ikimpa zaidi ya milioni mia sita huku akipata mshahara mnono kuzidi ule wa Simba sc na kuwazidi kete mabosi wa Simba sc ambao mwishoni baada ya kujua kuwa anatarajia kujiunga na Yanga sc walipanga kubadili maamuzi ili asaini Simba sc.

banner

Chama ni moja ya mastaa wakubwa wa soka nchini akijenga jina kubwa miongoni mwa mashabiki kutokana na ufundi wake huku akiisaidia Simba sc kutwaa mataji mbalimbali ya ndani ya nchi na kimataifa akiisaidia kufanya vizuri kiasi cha kuwa moja ya klabu tishio katika miaka saba aliyokaa kikosini humo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited