Home Soka Simba Mwendo wa 4G

Simba Mwendo wa 4G

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kushinda mechi ya jana kwa mabao manne,Leo tena timu hiyo imeshuka dimbani na kuibuka na ushindi huo huo wa mabao manne dhidi ya Platnum Stars ya nchini Afrika  kusini katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya huko Afrika ya kusini.

Mabao ya Simba yalipatikana kupitia kwa Chama dakika ya 11 na 58 huku kiungo msudani Eldin Shiboub akifunga kwa penati dakika ya 13 kabla ya Mzamiru Yassin kufunga bao la mwisho dakika ya 87 huku wenyeji wakifanikiwa kupata goli dakika ya 75 kwa mkwaju wa penati.

Simba bado inaendelea na maandalizi ya msimu mpya kwa kucheza mechi mbalimbali baada ya jana kucheza na Orbet Tvet na tarehe 27 siku ya jumamosi itacheza na Township Rollers ya Botswana.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited