Home Makala Berkane Yatanguliza Matumaini Fainali Cafcc

Berkane Yatanguliza Matumaini Fainali Cafcc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Rs Berkane imetanguliza matumaini ya kutwaa taji la kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga timu ya Simba sc kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya fainali uliofanyika nchini Morocco katika uwanja wa Manispaa ya mji wa Berkane.

Berkane waliingia katika mchezo huo na kuweka presha kubwa kwa Simba sc wakishambulia kwa nguvu na kupata mabao mawili ya haraka haraka wakianza na bao la kichwa kutoka kwa kiungo Mamadou Camara dakika ya 8 ya mchezo.

Wakati Simba Sc wakijiuliza walijikuta wanafanya makosa baada ya Moussa Camara kutoa pasi ngumu kwa Yusuph Kagoma ambaye aliupoteza mpira na kufungwa bao la pili na mshambuliaji Oussama Lamlaoui dakika ya 14 ya mchezo.

banner

Simba sc waliendelea kutaabika na kasi ya Berkane ambapo kipindi cha pili kocha Fadlu Davis alimuingiza Valentino Nouma kuchukua nafasi ya Kibu Denis ambapo alianza kucheza na mabeki watatu wa kati.

Shukran za pekee kwa mwamuzi wa njia ya video (Var) ambaye alikataa bao la tatu la Berkane ambalo kama lingekubaliwa lingeongeza mlima kwa Simba sc.

Mpaka filimbi ya mwisho Simba Sc hawakupiga shuti lolote lililolenga lango huku wakimilika mpira kwa asilimia 47 na kufanikiwa kupiga pasi 358 dhidi ya 381 za Rs Berkane.

Simba sc sasa inapaswa kupindua meza katika mchezo wa marudiano visiwani Zanzibar Mei 25 2025.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited