Home Soka Pazia Ligi Kuu Bara Kufunguliwa Leo

Pazia Ligi Kuu Bara Kufunguliwa Leo

by Sports Leo
0 comments

Pazia la ligi kuu Tanzania bara litafunguliwa leo ambapo mechi tano zitapigwa katika viwanja tofauti tofauti huku kila timu ikiahidi kufanya vizuri katika mechi hizo.

Namungo iliyopanda daraja msimu huu itakua nyumbani kuwakabili ndanda ya huko huko Mtwara katika uwanja wa Majaliwa huku Kagera sugar watakua na kibarua kigumu mkoani Mara mbele ya Biashara Fc na timu ya Polisi Fc iliyo chini ya Selemani Matola itawakaribisha Coastal Union.

Pia kwa upande wa kanda ya ziwa Mbao Fc watakipiga na Alliance Fc mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka mkoani humo ikizingatiwa timu zote zinatokea eneo la Ilemela jijini humo.

banner

Timu kubwa katika ligi zitacheza wiki ijayo baada ya kuwa na mechi za kimataifa ambapo Kmc jana ilitolewa rasmi katika michuano ya kombe la shirikisho huku Yanga na Azam zikitupa karata leo na kesho Simba itawakaribisha Ud songo katika michuano ya Klabu bingwa Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited