Home Soka Yanga Inogile

Yanga Inogile

by Sports Leo
0 comments

Kambi ya timu ya Yanga jijini Mwanza imezidi kunoga kufuatia kurejea kwa wachezaji ambao awali waalikua hajasafiri na timu kwa sababu mbalimbali.

Wachezaji hao ni Abdulaziz Makame na Metacha Mnata pamoja na Issa Bigirimana aliyekuwa mgonjwa tayari wamejiunga na kikosi hapa Mwanza na baada ya mazoezi ya siku mbili Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo.

“Kwa kawaida naiandaa timu kwa ajili ya mchezo uliokuwa mbele yangu, hadi sasa timu iko vizuri na tayari kwa mchezo dhidi ya Mbao FC. Tunawaheshimu Mbao ni timu nzuri, lakini na sisi ni wazuri pia na tumejiandaa kwa ushindi”Alisema Zahera.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited