Home Soka Yanga Nje Caf

Yanga Nje Caf

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Yanga imetolewa nje ya michuano ya kimataifa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Pyramids fc katika mechi ya marudiano ya hatua ya kufuzu makundi iliyofanyika nchini Misri.

Yanga hapo awali ilikubali kipigo cha mabao 2-1 nchini katika uwanja wa Ccm Kirumba na licha ya kujitahidi kucheza soka hapo jana ilijikuta ikiruhusu bao la kwanza dakika ya 27 ya mchezo lililofungwa na Erick Traore baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa Farouk shikalo.

Dakika kumi kabla ya filimbi ya mwisho Farouk aliipatia Pyramids bao la pili akimalizia krosi ya El said na dakika za mwisho za mchezo wenyeji walipata bao la tatu el said aliipatia bao pyramids baada ya kupokea krosi ya chini ya  John Antwi.

banner

Yanga wamekosa nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kuruhusu jumla ya mabao 5-1 kwa michezo miwili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited