Home Soka Kocha Simba Anukia Polokwane City

Kocha Simba Anukia Polokwane City

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kocha wa Simba Patrick Aussems kuwasili leo usiku habari za ndani zinadai Aussems hakuwa Belgium kwao, bali alikuwa nchini Afrika ya kusini kuzungumza na Klabu ya Polokwane city kwa ajili ya kuifundisha klabu hiyo.

Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha kikao cha kumtaka ajieleze kocha huyo baada ya kuwasili juzi  usiku huku Uongozi wa Simba sc umechukizwa na jambo hilo na unataka ajieleze kwa nini aliondoka bila taarifa.

Inadaiwa kocha huyo baada ya kuona kuna hali ya kutoaminika katika klabu hiyo ameamua kutafuta timu nyingine na tayari ameshakutana na bosi wa Polokwane city kwa mazungumzo taarifa zinasema kocha huyo anaweza kujiunga na timu hiyo mwisho mwa mwezi huu endapo atatimuliwa.

banner

Taarifa za kocha huyo kufanya mazungumzo na timu hiyo zimeifanya klabu ya Simba kusitisha kwa muda kumtimua ili kuangalia kama kocha huyo atajiuzulu yeye mwenyewe ili kuepusha gharama za kumlipa kama fidia ya kuvunja mkataba ambapo zaidi ya milioni 200 zingetumika kumlipa kocha huyo.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited