Home Soka Mbeligiji Alamba Miezi 18 Yanga

Mbeligiji Alamba Miezi 18 Yanga

by Sports Leo
0 comments

Kocha Luc Eymael na msaidizi wake Reidoh Berdien wamesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuitumikia klabu hiyo yenye makao makuu mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es salaam.

Makocha hao wamesaini kandarasi hizo mbele ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Dk Mshindo Msolla aliyeambatana na Mwanasheria wa klabu hiyo Saimon Patrick.

Makocha hao kwa pamoja wametakiwa kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa wa ligi kuu na kombe la FA ili kufanikisha timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa.

banner

Licha ya wadau wengi wa michezo kutegemea Charles Mkwasa kuendelea kuifundisha klabu hiyo kama kocha msaidizi,taarifa zinadai timu hiyo ipo kwenye mazungumzo na Mecky Mexime kuja kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited