Home Soka Samatta Aisaidia Villa Kutinga Fainali

Samatta Aisaidia Villa Kutinga Fainali

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa kitanzania Mbwana Samata jana aliisaidia klabu yake mpya ya Aston Villa kutinga fainali ya michuano ya Carabao Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester city katika uwanja wa Villa Park.

Samatta aliyekua akicheza mechi ya kwanza,alianzishwa kama mshambuliaji wa kati katika mfumo wa washambuliaji watatu huku akisaidiwa kwa ukaribu na staa wa timu hiyo Jacky Grealish aliyecheza kama kiungo mshambuliaji.

Villa iliandika bao la kwanza dakika ya 12 likifungwa na Matt Tagert na wageni walisawazisha kupitia kwa Kelechi Iheanacho kabla ya Trezeguet kufunga bao la pili dakika za mwishoni akimalizia krosi ya Ahmed Elmohamady.

banner

Villa watakutana na mshindi kati ya Man united ama Manchester city baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao  3-1 baada ya awali kutoka suluhu ugenini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited