Home Makala Sven, Ratiba Ya Ligi Inanibana

Sven, Ratiba Ya Ligi Inanibana

by Sports Leo
0 comments

Kocha mkuu wa Simba Sc ,Sven Vanderbroeck amelalamika kutokana na ratiba  ya ligi kumbana kwa sasa wanatakiwa kujiandaa kikamilifu kwani kwa siku nane kuanzia jana watakuwa na mechi tatu za ligi ambazo ni ngumu kwao.

Sven amesema kuwa mechi hizo tatu zitamnyima muda wa kukaa na wachezaji wake kwa ajili ya kufundishana na kurekebisha makosa ambayo watakuwa wamefanya kwenye mechi zao za nyuma ikiwa na kuruhusu mabao kwenye lango lao.

Mechi ya kwanza katika siku nane walizonazo Simba ni dhidi ya Namungo Fc ya Lindi ambayo walicheza jana na kuondoka na pointi tatu baada ya hiyo itapambana tena Februari Mosi dhidi ya Coastal Union kisha mechi yao ya mwisho kwenye mzunguko wa kwanza itakuwa Februari 4 dhidi ya Polisi Tanzania.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited