Habari njema ni kuwa kiungo mshambuliaji Bernard Morrison anaweza kurejea baada ya hali yake kuimarika kwa haraka baada ya kupata majeraha ya mguu.
Morrison alipata majeraha kabla ya mchezo dhidi ya Simba ambao alicheza kwa dakika 56 kabla ya kutolewa kumpisha Patrick Sibomana huku akiwa amefunga bao moja na ushindi kwa njia ya faulo.
Mchezo dhidi ya Namungo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na ukweli kuwa Namungo ni moja ya timu bora msimu huu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji matokeo ya ushindi hasa baada ya kupoteza mchezo uliopita ili kuwania nafasi ya pili ya ligi kuu kutengeneza mazingira mazuri ya kucheza michuano ya kimataifa.