Home Soka Mil.80 Kumng’oa HD Msimbazi

Mil.80 Kumng’oa HD Msimbazi

by Sports Leo
0 comments

Unaambiwa muda wowote kiungo Hassan Dilunga anaweza kumwaga wino kuitumikia klabu ya Yanga baada ya mabosi wa klabu hiyo kumtengea dau la milioni 80 ili arudi jangwani.

Inadaiwa tayari matajiri hao wameshafanya mazungumzo na Dilunga na amekubali kusaini kwa dau hilo japo bado haijawekwa wazi ni lini atasaini katika klabu hiyo.

Mabosi hao wanaona ni bora kumrudisha Dilunga Jangwani badala ya kumsainisha Said Ndemla ambaye amekulia mitaa ya Msimbazi.

banner

Dilunga aliwahi kuichezea Yanga chini ya kocha Hans Van De Pluijm kabla ya kutemwa kufuatia kuporomoka kiwango.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited