Coastal Union ambao watamenyana leo Octoba,3 na Yanga Sc uwanja wa Mkapa jijini Dar-es-salaam wamejihakikishia kuchukua pointi tatu muhimu leo katika mchuano huo utakaochezwa majira ya saa 1:00 usiku.
Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo vizuri na wanaamini watapata pointi tatu kwenye mchezo huo kwani lengo ni kushinda na kunyakua alama tatu muhimu.
Coastal Union inakutana na Yanga ikiwa imepoteza mechi mbili ndani ya ligi na kupata sare moja na kushinda mchezo mmoja huku Yanga ikiwa imeshinda mechi tatu na kupata sare moja mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa Mkapa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.