Home Makala Kocha Yanga Asitishiwa Mkataba

Kocha Yanga Asitishiwa Mkataba

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa Yanga Sc umefikia makubaliano ya kumfuta kazi kocha mserbia,Zlatko Krmpotic jana Octoba 3,ambaye alichukua mikoba ya Luc Eymael.

Zlatko amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za ligi kuu bara ambapo katika mechi hizo ,ameshinda mechi nne na kutoa sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.

Taarifa hii imetolewa usiku wa kuamkia leo ambapo klabu ya Yanga imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya pande zote mbili mara baada ya kocha huyo kutoka kukiongoza kikosi hicho katika raundi ya tano ya ligi kuu bara ambapo waliichapa Coastal Union mabao 3-0 uwanja wa Mkapa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited