Klabu ya Yanga sc ipo mbioni kuwasajili washambuliaji Adam Adam wa Jkt Tanzania pamoja na Jafary Kibaya wa Mtibwa sugar katika usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kuanza Desemba 15 mpaka Januari 15.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya klabu hiyo kocha Cedric Kaze anahitaji mshambualiaji wa ndani ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo hivyo kamati ya usajili tayari imepeleka majina ya wachezaji hao kwa ajili ya kuchagua mmoja.