Klabu ya Simb imeibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mabao ya Simba Yalifungwa na John Boko aliyefunga matatu dakika za 25,27 na 37 huku Hassan Dilunga alifungua akaunti kwa bao la dakika ya 7 baada ya kuvunja mtego wa kuotea na mabao mengine yalifungwa na Cletous Chama dakika za 60 na 85 pamoja na Bernad Morrison aliyefunga dakika chache kabla ya mapumziko.
Simba sc sasa imefikisha alama 23 ikiwa katika nafasi ya tatu huku Yanga sc na Azam fc zikibaki kileleni mwa ligi kuu nchini.