Kocha msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema nyota watatu hawatakuwepo kwenye mechi dhidi ya Simba Leo Julai 15 saa 1:00 usiku ambao ni Prince Dube anayesumbuliwa na majeraha huku akisema Wengine ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Agrey Morris ambao wanasumbuliwa na malaria.
Azam fc itawakosa mastaa hao wakati itakapokua inatafuta alama tatu ili kumaliza katika nafasi ya pili ya ligi kuu nchini ambapo Simba sc tayari ni mabingwa wa ligi msimu huu kwa mara ya nne mfululizo.