Mazungumza ya kuongeza mkataba mpya baina ya klabu ya Al Ahly na mshambuliaji Percy Tau yamefikia pazuri ambapo staa huyo anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga klabuni hapo kwa miaka mitatu mingine huku akitarajiwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi barani Afrika.
Katika mkataba huo mpya Tau atakua anatia mfukoni Mshahara wa dola milioni 5.13 katika misimu mitatu (3) ijayo ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 13 za Kitanzania.
Mishahara ya kila mwaka akiwa na klabu hiyo ilikuwa ni dola milioni 1.2 ikiwa ni zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kwa Mwaka na sasa itaongezeka hadi dola milioni 1.3 (zaidi ya shilingi Bilioni 3.3 za Kitanzania) katika mwaka wa kwanza, dola milioni 1.4 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3.7) kwa mwaka wa pili na dola milioni 1.6 (zaidi ya Shilingi Bilioni 4) kwa mwaka wa tatu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kwenye Mkataba huo wa Tau inamaanisha mwaka wa mwisho atakuwa anapokea mshahara wa shilingi Milioni 340 kwa mwezi ambapo kwa wiki atakuwa analamba Milioni 85,Milioni 12 kwa siku.