Klabu ya Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan imethibitisha kuachana na kocha wake Florent Ibenge baada ya miaka mitatu ya kufanya kazi na klabu hiyo kubwa nchini humo.
Timu hiyo imeachana na Ibenge baada ya makubaliano ya pande mbili kufuatia mkataba wa kocha huyo kufika mwishoni na kuamua kitoongeza tena.
Taarifa za ndani kutoka nchini Tanzania zinadai kuwa kocha huyo atatangazwa kuwa kocha wa Azam FC siku chache zijazo baada ya kukubali ofa ya vigogo hao wa Chamazi.
Kocha huyo alikua hapa nchini siku chache zilizopita ambapo inasemekana alifanya mazungumzo na mabosi wa Azam Fc na kukubaliana kila kitu ambapo ameshapiga mpaka picha za utambulisho klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ibenge sasa anatarajiwa kutambulishwa muda wowote klabuni hapo kwa ajili ya kujiandaa mapema na msimu mpya wa ligi kuu nchini ambapo mabosi wa Azam Fc wanataka kurejesha makali yao baada ya msimu huu kitofanya vizuri.