Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limeboresha maslahi ya wachezaji wake wa timu ya Taifa hasa kuelekea katika mchezo muhimu wa kufuzu Afcon ambapo awali posho ya siku ilikuwa Sh1.2 milioni ya Tanzania (Sh1.8 milioni ya Uganda) na sasa imeongezeka kufikia Sh1.8 milioni ya Tanzania.
Kutokana na mabadiliko hayo mapya pia bonasi ya mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu Afcon nazo zimebadilika ambapo Uganda kama itaifunga Niger na kufanikiwa kufuzu kila mchezaji na benchi la ufundi atabeba Sh12 milioni ya Tanzania.
Mechi za mwisho kundi F kufuzu Afcon 2024 zitapigwa kesho saa 4:00 usiku katika viwanja viwili tofauti ambapo Tanzania (Taifa Stars) ikiwa ugenini Algeria itasaka ushindi au sare kujihakikishia nafasi ya kufuzu huku Niger ikiikaribisha Uganda.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tanzania ina pointi saba katika kundi hilo ambapo ushindi au sare itafuzu huku Uganda ikijitaji ushindi wa mabao mengi huku ikiiombea Taifa Stars kupoteza mchezo huo.