Kiungo wa klab ya Yanga, raia wa Uganda Khalid Aucho ameweka bayana Kuwa anahitaji kuondoka Klabuni hiyo iliyopo mitaa ya Twiga na Jangwani na hii ni baada ya kupokea ofa mpya kutoka moja ya klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa gazeti moja la michezo kiungo huyo Ameuomba Uongozi wa Yanga kutoongeza Mkataba unaoisha Mwishoni mwa msimu huu ambapo amevutiwa na ofa hiyo nono ya mamilioni ya fedha kutoka kwa waarabu.
Yanga sc bado hawajampa jibu staa huyo kama wanakubaliana na suala hilo ama watapandia juu ofa hiyo ili kumbakisha staa huyo kikosini kutokana na kuwa na mchango mkubwa hasa katika kujenga mashambulizi licha ya kuwa na spidi ndogo hasa katika kukaba timu inaposhambuliwa kwa kasi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.