Home Soka Azam Fc Yavunja Rekodi ya Yanga Sc

Azam Fc Yavunja Rekodi ya Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuvunja rekodi ya klabu ya Yanga sc ya kutofungwa mchezo wowote katika ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Yanga sc ilikua haijapoteza mchezo wowote katika michezo yake nane ya ligi kuu huku ikiwa haijaruhusu nyavu zake kuguswa na timu yeyote mpaka Azam Fc ilipofunga bao katika dakika ya 33 ya mchezo huo likifungwa na Gibril Sillah kwa shuti kali.

Yanga sc iliathirika mapema kipindi cha kwanza baada ya kulazimika kucheza pungufu baada ya Ibrahim Hamad Bacca kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Ahmed Arajiga kutokana na kucheza faulo akiwa mchezaji wa mwisho.

banner

Yanga sc pamoja na kuwa pungufu ilijitahidi kupata bao la kusawazisha lakini ilikosa umakini mara kadhaa ikikosa mabao ya wazi kupitia kwa Max Nzengeli na Nickson Kibabage dakika za karibia na mwisho wa mchezo huo.

Pamoja na kufungwa bado Yanga sc wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini wakiwa na alama 24 wakicheza michezo tisa huku Azam Fc wakisogea mpaka nafasi ya nne ya msimamo wakiwa na alama 21 katika michezo 10 ya ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited