Home Makala Azam Waibua Kifaa Zenji

Azam Waibua Kifaa Zenji

by Sports Leo
0 comments

UONGOZI wa Azam FC, unayofuraha kuwataarifu kuwa tumekamilisha taratibu za kumsajili kiungo mshambuliaji, Khleffin Hamdoun, kwa mkataba wa miaka minne akitokea Mlandege ya Zanzibar.

Huo unakuwa usajili wa kwanza kwa Azam FC kwenye dirisha dogo la usajili, likiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.

Hamdoun, aliyefikisha umri wa miaka 19 leo, amesaini mkataba rasmi wa kuitumikia Azam FC leo Jumatano usiku, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

banner

Mara baada ya kusaini mkataba huo, kiungo mshambuliaji huyo alielezea furaha yake ya kukamilisha taratibu ya kujiunga Azam FC huku akiahidi kushirikiana na wachezaji wenzake kuipa mataji timu hiyo.

Kiungo mshambuliaji huyo alionyesha kiwango kizuri akiwa na timu yake ya Mlandege ilipochuana na Azam FC juzi, jambo ambalo lilimvutia Cioaba na kuidhinisha asajiliwe haraka iwezekanavyo.

Nb:Taarifa kutoka Azam fc kupitia mtandao wa facebook wa klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited