Home Soka Aziz Ki Kuiwahi Simba sc Kesho

Aziz Ki Kuiwahi Simba sc Kesho

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kufanikiwa kuiwezesha nchi yake kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon) yatakayofanyika mwakani nchini Algeria staa wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki anatarajiwa kurejea nchini kesho na kuungana na mastaa wengine kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Simba Sc.

Aziz Ki amesaidia Burkina Faso kufuzu Afcon baada ya kuichapa Burundi kwa mabao 2-0 na kupata uhakika wa kushiriki Afcon kuanzia Januari 2025 nchini Algeria.

Kambi ya timu hiyo inatarajiwa kuvunjwa kesho jumanne na moja kwa moja staa huyo atarejea nchini kwa ajili ya kujiunga na wenzake kambini Avic Town kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba Sc utakaofanyika Oktoba 19 2024.

banner

Mastaa baadhi ambao hawakuitwa katika timu zao za Taifa kama Yao Kouasi Attouhoula,Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua wapo tayari wanaendelea na maandalizi ya mchezo huo chini ya mwalimu Gamondi.

Aziz Ki tangu ajiunge Yanga sc amefanikiwa kuwa na mchezo mzuri anapocheza dhidi ya Simba Sc ambapo mpaka sasa amefanikiwa kuwafunga mabao 3.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited