Home Soka Aziz Ki Kusalia Yanga Sc

Aziz Ki Kusalia Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki anatarajia kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kusalia klabuni hapo baada ya kufikia makubaliano na mabosi wa klabu hiyo wiki iliyopita.

Azizi Ki anamaliza mkataba wake wa hivi sasa mwishoni mwa mwezi huu ambao ameutumikia kwa miaka miwili tangu asajiliwe msimu wa 2022 akitokea Asec Mimosas.

Mabosi wa Yanga sc inabidi wajipongeze kufanikiwa kumbakisha staa huyo ambaye ni mfungaji bora wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu akifunga mabao 21 na kutoa assisti saba na hivyo kuzivutia klabu nyingi barani Afrika.

banner

Kusaini kwa mkataba huo kunahitimisha tetesi za staa huyo kutakiwa na klabu za Mamelod Sundown,Al ahly na Pyramids Fc ambazo zilikua zinammezea mate.

Yanga sc wamelazimika kutoa ofa nono kwa star huyo iliyovunja recoding ya usajili klabuni hapo wakipata nguvu zaidi kutokana na sapoti kubwa wanayoipata kutoka kwa tajiri Gsm sambamba na mikataba mikubwa ya udhamini klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited