Aliyekua winga wa klabu ya Simba sc Peter Banda amejiunga na klabu ya Nyassa Big Bullets ya nchini kwao Malawi kwa mkataba mfupi wa miezi minne baada ya kuachana na klabu ya Simba sc siku chache zilizopita.
Banda amedumu Simba sc kwa misimu miwili ambapo hivi sasa ripoti ya mwalimu Roberto Oliveira ilionyesha kuwa hahitaji huduma yake klabuni hapo ambapo uongozi ulilazimika kufikia makubaliano ya kumalizana nae kwa kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande mbili.
Licha ya kusajiliwa kwa matarajio makubwa klabuni hapo miaka miwili iliyopita staa huyo hakufanikiwa kucheza soka la hali ya juu kutokana na kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Inavyosemekana kuwa Banda amejiunga na Nyassa ili kupata muda wa kucheza ambapo dirisha dogo la mwezi januari anaweza kutafuta timu nyingine ya kujiunga nayo.