Home Makala Beki Katili Atambulishwa Simba sc

Beki Katili Atambulishwa Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imekamilisha usajili wa beki Mohamed Ouatarra kutoka klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Serge Pascal Wawa ambaye amepewa mkono wa kwaheri na sasa amejiunga na klabu ya Singida Big Stars.

Awali Simba sc ilihusishwa na beki Hervé Ngomo wa CotonSports ya nchini Cameroon lakini ujio wa kocha mpya Zoran Maki ulibadili usajili huo ambapo alimtaka Ouatarra ambaye anamfahamu vizuri na hivyo klabu hiyo kuachana na Ngomo.

Kwa sasa klabu ya Simba sc ipo katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini Misri ambapo pia mchezaji huyo nae moja kwa moja ameungana na kikosi kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini huku pia wakitarajiwa kucheza mchezo wa utambulisho wa wachezaji siku ya August 8 na siku tano baadae watavaana na Yanga sc katika kufungua dimba la msimu mpya nchini katika mchezo wa ngao ya jamii.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited