Home Soka Beki Kisiki Atua Simba Sc

Beki Kisiki Atua Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imetangaza kukamilisha usajili wa beki Abdulrazaka Mohamed Hamza kwa mkataba wa miaka miwili akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya SuperSports United ya nchini Afrika ya kusini.

Hamza ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kati sambamba na kiungo mkabaji ambapo kwa muda tofautitofauti amewahi kuzichezea klabu za Mbeya City kisha akatua Kmc na kisha Namungo Fc ambapo alicheza kwa msimu mmoja na akajiunga na klabu ya Supersports United ya nchini Afrika ya kusini.

Simba sc imesajili mchezaji huyo baada ya kuona kuna uwezekano wa kumkosa Lameck Lawi ambaye bado klabu yake ya Coastal union inaweka ngumu kumuachia na endapo atapatikana basi uwezekano mkubwa beki Hussein Kazi akatolewa kwa mkopo ama kuachwa kabisa ili kutoa nafasi kwa Lawi na Hamza.

banner

Simba sc imefanya fumua fumua ya kikosi ili kuleta nguvu mpya baada ya kuukosa ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini kwa miaka mitatu mfululizo ambapo sasa mabosi wa klabu hiyo wameamua kuajiri vijana zaidi ili kuwatumia kwa muda mrefu akiwemo Hamza mwenye miaka 21.

Tayari kwa upande wa safu ya ulinzi klabu hiyo imewatema Kennedy Juma huku ikimuuza Henock Inonga na sasa inasajili majembe mapya ili kurejesha heshima yake iliyopotea nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited