Beki wa kati wa timu ya Nkana kutoka Zambia,Musa Mohammed amekiri kufanya mazungumzo na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kutokana na mkataba wake unaokaribia kuisha hivi karibuni.
Mkenya huyo ambaye ni nyota wa zamani wa Gor Mahia aliwahi kucheza ndani ya Kf Tirana ya nchini Albania kabla ya mwaka 2018 ambapo alijiunga na Nkana ya Zambia.
Musa amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo baina yake na viongozi wa Yanga na iwapo mipango itaenda sawa basi yupo tayari kujiunga nao.
“Yanga kweli nimefanya nao mazungumzo kupitia wakala wangu ambaye aliongea nao kila kitu na alinieleza walipofikia ingawa mambo hajakaa sawa kutokana na janga la Corona,ila ninayo nafasi kubwa ya kujiunga nayo kwa sababu ni timu kubwa na ninaifahamu vizuri” alisema Musa
Aliongeza kuwa mkataba wake unaisha mwezi juni na hivyo kuna uwezekano kutua Jangwani hivyo wachezaji wa Simba Sc Kama Kagere na Bocco wasitegemee urahisi ikiwa atakuwepo ndani ya Yanga Sc.