Home Makala Cas Yairudisha Yanga Sc TFF

Cas Yairudisha Yanga Sc TFF

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Yanga Sc ya imerudishwa kwenye ngazi za maamuzi za ndani katika kesi yake ya awali iliyoifungua kwenye Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS) dhidi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi (TPLB) na Simba Sc.

Katika kesi hiyo,Yanga sc ilikua ikiomba kupewa alama 3 na mabao 3 sambamba na kuitaka CAS izuie tarehe nyingine ya mchezo huo isipangwe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa.

banner

Yanga sc ilifungua kesi hiyo baada ya Simba Sc kugomea mchezo wa baina yao maarufu kama “Derby ya Kariakoo” uliokuwa uchezwe Machi 8, 2025 hali iliyopelekea mabosi wa klabu hiyo kupeleka kesi hiyo CAS wakigomea mechi hiyo kuchezwa tena huku wakidai alama 3 na magoli matatu.

Kwa mujibu wa barua ya CAS ilitolewa Mei 01, 2025 kwenye hukumu hiyo CAS imesema haina uhalali wa kisheria wa kusikiliza kesi hiyo yenye kumbukumbu CAS 2025/A/11298 kati ya Yanga Sc Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kabla halijapitia kwenye mamlaka za kisheria za TFF.

Hivyo CAS imelifuta rasmi na kuliondoa shauri la Yanga kwenye mfumo wake wote wa mashauri yaliyowahi kuletwa na kubainisha kuwa maagizo haya hayana gharama zozote za ziada ambazo zinapaswa kulipwa na klabu hiyo.

Hivyo basi klabu hiyo inatakiwa irudishe mashtaka yake TFF katika kamati zinazosimamia ligi kuu ambapo kama haitaridhika na uamuzi wa kamati hizo ndio inaweza kwenda Fifa kisha kukata rufaa Cas.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited