Home Makala Chama Arejea Simba sc

Chama Arejea Simba sc

by Dennis Msotwa
0 comments

Baada ya kukosa michezo mitatu akitumikia adhabu ya kufungiwa na bodi ya ligi kwa kosa la kutosalimiana na wachezaji wa Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu wa Octoba 23 iliyozikutanisha Simba sc na Yanga sc sasa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Cletous Chama amerejea katika kikosi hicho baada ya kumaliza adhabu hiyo.

Chama kwa mujibu wa taarifa kutoka bodi ya ligi kuu nchini alifungiwa michezo mitatu ambapo aliikosa michezo dhidi ya Singida Big Stars ugenini ambapo Simba sc ilipata sare ya 1-1 kisha mchezo dhidi ya Ihefu Sc ambao Simba sc walishinda 1-0 na dhidi ya Namungo Fc ambao pia Simba sc walishinda 1-0.

Sasa Chama anarejea kikosini katika mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting na tayari kocha Juma Mgunda amethibitisha kuwa atamtumia staa huyo kikosini humo wakati akiongea na waandishi wa habari mapema hivi leo ikiwa ni takwa la kikanuni kuelekea mechi za ligi kuu nchini.

banner

“Kesho atakuwa sehemu ya kikosi” Alisema kocha wa Simba SC, Juma Mgunda akijibu swali kuhusu kiungo wake Clatous Chama kuelekea mechi yao ya kesho dhidi ya Ruvu Shooting.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited