Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umekanusha taarifa zilizoenea kuwa beki wao tegemeo ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya Tanzania Bakari Mwamnyeto Nondo amesajiliwa na klabu ya Simba na akatolewa kwa mkopo wa miezi 6 klabuni hapo.
Awali taarifa zilidai kuwa timu hiyo imemuuza beki kwenda Simba sc huku wakikubaliana kubakia klabuni hapo hadi mwishoni mwa msimu huu.
Uongozi umesisitiza taarifa hizo ni za uongo, Nondo ni Mchezaji wao na hawajaafikiana na klabu yeyote kuhusu uhamisho wake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.