Wachezaji wa Juventus wote wamelazimika kujitenga kwa ridhaa baada ya kiungo wa timu hiyo,Weston McKennie kuthibitika kukutwa na Virusi vya Corona.
Weston ambaye ndiye mchezaji wa pekee wa Juventus alijiunga na klabu hiyo katika usajili wa dirisha hili akitokea Schalke ya Ujerumani.
Kukutwa na maambukizi hayo ya Virusi vya Corona ndani ya Juventus kumewapa hofu wachezaji wote wa klabu hiyo hata kujitenga kwaajili ya kuchukua tahadhari kwani ndiye pekee aliyekutwa na virusi hivyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Taarifa hizo zimekuja mara baada ya siku moja kupita toka Cristian Ronaldo wa Juventus athibitike pia kuambukizwa virusi hivyo akiwa kwao Ureno na sasa amejitenga chini ya uangalizi maalum wa madaktari.