Home Makala Dube Aitwa Timu ya Taifa Zimbabwe

Dube Aitwa Timu ya Taifa Zimbabwe

by Dennis Msotwa
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Prince Mpumelelo Dube ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe ijayojiandaa na michezo ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025 dhidi ya Kenya na Cameroon.

Kocha Michael Nees amemjumuisha Dube katika kikosi hicho baada ya staa huyo kuonyesha kiwango bora sana tangu ajiunge na klabu ya Yanga sc akitokea Azam Fc.

Dube tangu ajiunge na Yanga sc amefunga bao takribani katika kila mchezo aliocheza akianza na michezo ya kitafiki nchini Afrika ya kusini alipofunga dhidi ya Ts galaxy na Kaizer Chiefs Fc na pia alifunga bao katika mchezo dhidi ya Azam Fc wa fainali ya Ngao ya Jamii huku akitoa pasi ya bao kwa Maxi Nzengeli katika mchezo dhidi ya Simba Sc.

banner

Dube ataungana na washambuliaji wengine kama Tawanda Chirewa (Wolverhampton Wanderers, England), Tinotenda Kadewere (Nantes, France), Tymon Machope (Simba Bhora), Douglas Mapfumo (Polokwane City, South Africa), Walter Musona (Simba Bhora).

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited