Home Makala Duchu,Simba sc Wamalizana

Duchu,Simba sc Wamalizana

by Sports Leo
0 comments

Taarifa kutoka klabu ya Simba sc zinasema kuwa klabu hiyo tayari imemalizana na beki David Kameta Duchu ambaye mkataba wake unafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu kwa kutomuongezea mkataba mpya.

Duchu alisajiliwa na Simba sc akitokea Lipuli Fc lakini kutokana na changamoto ya kupata nafasi katika kikosi hicho ilimlazimu kutolewa kwa mkopo kwenda klabu ya Geita Gold Fc ambapo ndipo alipo mpaka sasa.

Baada ya Simba sc kuamua kutomuongezea mkataba beki huyo aliye katika kiwango bora kabisa kwa sasa,inatarajiwa kuwa atasaini mkataba mpya wa kujiunga rasmi na klabu ya Geita Gold Fc ambayo kwa sasa anaichezea kwa mkopo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited