Mshambuliaji mpya wa Yanga, Farid Mussa ameanza mazoezi rasmi leo Agosti 19 na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi nyingine za ushindani za msimu wa 2020/2021.
Farid amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Yanga Sc akitokea kwenye klabu ya CD Tennerife kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake.